
Wanajeshi wasiopungua 13 wa Libya wameuliwa na magaidi ndani na pambizoni mwa eneo la mashariki mwa mji wa Benghazi.
Afisa mmoja wa jeshi la Libya, Miloud al Zawi ametangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, wengi wa wanajeshi hao wameuawa katika miripuko ya mabomu yaliyotegwa ardhini na makundi ya kigaidi.
Shirika la habari la Libya LANA limesema kuwa, wanajeshi hao wameuawa katika mapigano ya nyakati tofauti, wakati walipokuwa wakiendesha operesheni za kupambana na wanamgambo wenye silaha huko Benghazi.
Afisa huyo wa kijeshi ameongeza kuwa, jeshi la Libya limeendelea kupata ushindi ikiwa ni pamoja na kukomboa kiwanda kimoja kikubwa katika maeneo hayo. Amesema, hivi sasa jeshi hilo linaendesha operesheni ya kudhibiti kambi moja ya kijeshi kwenye eneo hilo.
Amesema, mapigano yataendelea na jeshi halitosita hadi yatakapokombolewa maeneo yote yanayodhidibitiwa na makundi ya kigaidi.
No comments:
Post a Comment