
Katika taarifa, Wizara ya Ulinzi ya China imesema Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Chang Wanquan amemfahamisha mwenzake wa Marekani Ash Carter walipokutana Kuala Lumpur, Malaysia siku ya Jumanne kuwa Washington haipaswi kuchukua hatua zozote zinazoweza kuhatarisha usalama na mamlaka ya kujitawala China. Oktoba 27 meli ya kivita ya Marekani, USS Lassen iliingia karibu na visiwa vya Spratly, ambavyo Wachina wanaviita Nansha, hatua ambayo China imeitaja kuwa ni ya kichokozi.
China inasisitiza kuwa visiwa hivyo ni milki yake ingawa nchi za eneo ambazo ni Japan, Ufilipino, Malaysia, Taiwan, Brunei na Vietnam zinadai pia umiliki wa visiwa hivyo. Visiwa vya Spratly vinaaminiwa kuwa na utajiri wa mafuta na gesi mbali na umuhimu wake wa kistratijia.
No comments:
Post a Comment