Thursday, 5 November 2015

UCHAGUZI WA UGANDA KUFANYIKA FEBRUARI 28, 2016


Tume ya Uchaguzi ya Uganda imetangaza kuwa, uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utafanyika tarehe 28 mwezi Februari mwakani. Tangazo la Tume ya Uchaguzi ya Uganda lilitolewa jana limeeleza kwamba, tarehe hiyo imeainishwa kwa ajili ya kufanyika uchaguzi wa Rais na ule wa Bunge. Tayari tume hiyo imeidhinisha majina ya wanasiasa wanane wanaowania kiti cha urais akiwemo Rais Yoweri Museveni, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uganda Amama Mbabazi na Daktari Kizza Besigye. Rais Yoweri Museveni amesema kuwa, wagombea urais wanaoshindana naye kwenye uchaguzi mkuu ujao hapo mwakani si tishio kwake. Ameongeza kuwa, yeye na chama chake cha NRM wana imani watapata ushindi katika uchaguzi huo. Rais Museveni amesema kama ninavyomnukuu, "Nasikia watu wakizungumza kuhusu kupiga vita ufisadi. Utawezaje kukabiliana na ufisadi ilhali tunasikia ukiomba huyu na yule wajiunge na wewe?”Rais Museveni amekuwa madarakani nchini Uganda tangu mwaka 1986.

No comments:

Post a Comment