HISTORIA

MJUE RAIS WA AWAMU YA TANO WA TANZANIA


Dr.John Joseph Pombe Magufuli alizaliwa mnamo tarehe 29 Oktoba 1959 wilayani Chato Mkoani Kagera hapa nchini Tanzania.

Kielimu, daktari Magufuli ana Stashahada ya elimu ya sayansi akibobea kwenye masomo ya Kemia, Hisabati.

Pia Magufuli ana shahada ya umahiri wa Sayansi na shahada ya uzamivu ya kemia.

Aidha daktari Magufuli amewahi kufundisha katika shule ya sekondari Sengerema miaka ya themanini kisha akajiunga na mafunzo ya JKT .

Alipohitimu, daktari Magufuli na aliaanza kufanya kazi katika kiwanda cha ‘Nyanza Cooperative Union akiwa Mkemia kabla ya kuondoka hapo na kuwania ubunge.

Magufuli alianza mbio za ubunge mwaka 1995 katika jimbo la Chato na kushinda kisha akateuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa naibu waziri wa Miundombinu.

Katika uchaguzi wa Mwaka wa 2000 pia aligombea ubunge na kushinda na Rais Mkapa akamteua kuwa Waziri wa miundombinu.

Katika uchaguzi wa mwaka 2005 daktari Magufuli aligombea ubunge kwa mara ya tatu na kupita bila kupingwa.

Rais Kikwete alimteua kuongoza wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi na baadaye akamhamishia hadi wizara ya Mifugo na uvuvi.

Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya nne na Rais Kikwete alimrudisha katika Wizara ya Miundombinu na ujenzi.

Daktari Magufuli anachukuliwa kuwa ni mwanasiasa mwenye msimamo thabiti, mchapa kazi na asiye yumbishwa au hata kufuata upepo wa kisaisa.

Watanzaniania wanamkumbuka kwa usimamizi na ujenzi wa barabara na majengo thabiti.

Anakumbukwa kwa kuchukua hatua za kutoa amri za kubomolewa kwa majengo ya kifahari ambayo alihisi yalikiuka sheria za ujenzi.

Na alipokuwa waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Bwana John Magufuli alikwenda hadi bandari ya Dar-es-Salaam na kuizuia meli ya wachina iliyokuwa inashukiwa kufanya uvuvi haramu katika sehemu ya bahari ya Tanzania.

Na katika kinyang'anyiro cha nafasi ya Urais wa awamu ya tano mwaka 2015 Dk.Magufuli alitangazwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea wake wa kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu.

Daktari John Magufuli, alisajili asilimia 87 % ya kura za wajumbe, hiyo ikiwa ni kura 2104.

Daktari John Magufuli, aliwashinda wapinzani wake Bi Amina Salulm Ali na dakta Asha-Rose Migir.

Na katika kipindi cha kampeni Dr. Magufuli alikabiliwa na changamoto kubwa kutoka kwa wapinzani na hali hiyo ilipelekea kuleta hata ushindani mkubwa wakati wa uchaguzi uliofanyika octoba 25, 2015 na matokeo kutangazwa octoba 29 ambapo Dkt.Maguifuli aliibuka mshindi akimbwaga chini mpinzani wake wa karibu wa CHADEMA chini ya mwavuli wa UKAWA Mh.Edward Ngoyai Lowassa kwa tofauti ya asilimia 19, asilimia 58 kwa 39%
Na sasa Dr.Magufuli ndiye Rais wa awamu ya tano wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania mara baada ya kuapishwa Rasmi tarehe November 5, 2015.

No comments:

Post a Comment