WAGUINEA WAPINGA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE
Barabara za mji mkuu wa Guinea, Conakry jana zilikuwa uwanja wa maandamano ya wananchi waliokuwa wakipinga ukatili dhidi ya wanawake. Wanawake wengi wakiungwa mkono na wanaume pia jana waliandamana mjini Conakry kulalamikia na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake. Maandamano hayo yalifanyika kwa wito uliotolewa na asasi zisizo za kiserikali zinazojishughulisha na masuala ya haki za binadamu.Fatou Yansané, mmoja wa wajumbe wa jumuiya za kiraia nchini Guinea na miongoni mwa washiriki wa maandamano hayo alisema ni jambo la kusikitisha kwamba aghalabu ya matukio ya ukatili wa kijinsia unaofanyika nchini humo yanaachwa bila ya kushughulikiwa. Siku ya Jumanne, jumuiya na asasi za haki za binadamu zilionya kuhusu ongezeko la vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini Guinea na kulaani upuuzaji na uchukuaji hatua zisizo na taathira unaofanywa na serikali. Moussa Yero Bah, Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wanawake, Ustawi na Haki za Binadamu ya Guinea (FDH-G) amesisitiza juu ya ulazima wa kukomeshwa vitendo hivyo na kubainisha kuwa jumuiya yao itafuatilia hadi kuhakikisha serikali inapeleka bungeni muswada kuhusiana na suala hilo
No comments:
Post a Comment