Monday, 9 November 2015

MAGUFULI ABADILI UONGOZI MUHIMBILI



Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo amefanya ziara nyingine ya kushtukiza, wakati huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kufanyia mabadiliko usimamizi wa hospitali hiyo.Kiongozi huyo mpya amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.

WANAJESHI WA ISRAEL WAMUUA MWANAMKE MPALESTINA



Mwanamke mmoja Mpalestina ameuawa na vikosi vya utawala haramu wa Israel katika kituo cha upekuzi barabarani huko katika Ukingo wa Magharibi na hivyo kupelekea idadi ya Wapalestina waliouawa na Wazayuni katika kipindi cha siku 40 zilizopita kuwa 80.

Thursday, 5 November 2015

MAGUFULI AAPISHWA KUWA RAIS MPYA TANZANIA


John Pombe Magufuli sasa ndiye rais mpya wa taifa la Tanzania baada ya kuapishwa rasmi kufuatia ushindi wake wa wingi wa kura katika uchaguzi mkuu uliopita.

WAGUINEA WAPINGA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE

Barabara za mji mkuu wa Guinea, Conakry jana zilikuwa uwanja wa maandamano ya wananchi waliokuwa wakipinga ukatili dhidi ya wanawake. Wanawake wengi wakiungwa mkono na wanaume pia jana waliandamana mjini Conakry kulalamikia na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake.

CHINA YAIONYA MAREKANI

China imeionya vikali Marekani kuhusu kuchukua hatua ambazo zinaweza kuhatarisha mamlaka ya nchi hiyo ya mashariki mwa Asia. Onyo hilo limetolewa siku chache baada ya meli za kivita za Marekani kutekeleza kitendo cha uchokozi na kuingia katika maji ya kusini mwa Bahari ya China.

MJUE RAIS WA AWAMU YA TANO WA TANZANIA




Dr.John Joseph Pombe Magufuli alizaliwa mnamo tarehe 29 Oktoba 1959 wilayani Chato Mkoani Kagera hapa nchini Tanzania.

Kielimu, daktari Magufuli ana Stashahada ya elimu ya sayansi akibobea kwenye masomo ya Kemia, Hisabati.

UCHAGUZI WA UGANDA KUFANYIKA FEBRUARI 28, 2016


Tume ya Uchaguzi ya Uganda imetangaza kuwa, uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utafanyika tarehe 28 mwezi Februari mwakani. Tangazo la Tume ya Uchaguzi ya Uganda lilitolewa jana limeeleza kwamba, tarehe hiyo imeainishwa kwa ajili ya kufanyika uchaguzi wa Rais na ule wa Bunge. Tayari tume hiyo imeidhinisha majina ya wanasiasa wanane wanaowania kiti cha urais akiwemo Rais Yoweri Museveni,